KIMBWETANI

Habari Moto Moto

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya nchi hiyo haiwezi kutoa mikopo ya kimasomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini humo.

Kiongozi huyo alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.

“Nataka niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote” alisema.

Dkt Magufuli alisema hayo alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo katika Manispaa ya Iringa ambapo alisikiliza kero zao mbalimbali zikiwemo zinazohusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mazingira ya kusomea, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

Leave a comment